Viungo:
- Nyama
- Kitunguu
- Dhania
- Pilipili hoho
- Nyanya
- Chumvi
- Mafuta ya maji
Kuandaa:
- Kata nyama vipande vidogo kisha chemsha hadi iive.
- Weka mafuta ya maji kwa sufuria.
- Weka kitunguu na ukaange hadi iwe na rangi ya kahawia.
- Ongeza nyanya, dhania na pilipili hoho kisha kaanga hadi iive.
- Ongeza nyama iliyochemshwa kisha pika kwa moto wa chini hadi viungo vyote vichanganyikane.
asanti kwa kitoweo loe nimepata chakula cha kupika for a change from the common ugali na sukuma ama nyama boil
ReplyDeleteKaribu...brace yourself! Samaki wa mchuzi on the way.
ReplyDelete