Viungo:
- Minofu ya Samaki
- Kitunguu
- Kitunguu Saumu
- Curry poda
- Nyanya
- Nyanya ya mkebe
- Mafuta ya maji
- Maji ya Limau
- Chumvi
- Dhania
Kuandaa:
- Oka minofu ya samaki mpaka igeuke rangi ya kahawia.
- Epua kutoka kwa mafuta na uweke kando.
- Kaanga kitunguu kwa mafuta ya maji, kisha ongeza kitungu saumu na curry poda
- Punguza moto na ukoroge hadi kila kitu kichanganyikane.
- Ongeza nyanya, nyanya ya mkebe, chumvi na dhania. Kisha koroga. Pika kwa dakika moja.
- Ongeza samaki na maji ya limau. Pika kwa mda wa dakika kumi kwa moto wa chini.
No comments:
Post a Comment