Thursday, 13 October 2011

Maharagwe ya nazi

Viungo:
  1. Maharagwe
  2. Krimu ya nazi
  3. Kitunguu
  4. Nyanya
  5. Chumvi
  6. Pilipili
  7. Mafuta ya maji
Kuandaa:
  1. Chemsha maharagwe hadi iive.
  2. Weka mafuta ya maji kwa moto, kisha kakaanga kitunguu hadi kiwe rangi ya kahawia.
  3. Weka nyanya na ukaange hadi iive kisha ongeza chumvi.
  4. Ongeza krimu ya nazi na ukoroge hadi kila kitu kichanganyikane.
  5. Weka maharagwe na ukoroge.
  6. Ongeza pilipili na ukoroge.
  7. Ongeza maji kidogo na upike kwa moto wa chini kwa dakika kumi.
Pakua na ule na wali au chapati.

No comments:

Post a Comment