Viungo:
- Minofu ya Kuku wa kienyeji
- Nyanya mbili kubwa
- Kitunguu kimoja kikubwa
- Chumvi
- Mafuta ya maji
- Kitunguu Saumu
- Dhania
- Pili pili hoho
Kuandaa:
- Chemsha kwa mda wa lisaa limoja (Kuku wa kienyeji huwa wagumu na hitaji mda zaidi kufanya walainike).
- Ikishalainika na mchuzi umebaki, toa mchuzi na uweke kando.
- Kaanga kitunguu kwa mafuta maji hadi kiwe na rangi ya kahawia.
- Ongeza kitunguu saumu na chumvi na ukoroge hadi viungo vyote vichanganyikane.
- Ongeza nyanya, pili pili hoho na dhania na uongeze kukoroga hadi viungo vyote vichanganyikane.
- Ongeza kuku iliyochemshwa na upike kwa dakika kumi hivi.
- Ongeza mchuzi uliyoweka kando na uwache iive kwa dakika tano hivi.
No comments:
Post a Comment