Viungo:
- Kitunguu
- Kitunguu Saumu
- Mchele
- Tangawizi mbichi
- Nyama
- Mafuta ya Maji
- Nyanya ya mkebe
- Viazi
- Iliki
- Pilau Masala
- Mafuta ya maji
Kuandaa:
- Chemsha nyama kisha weka kando.
- Twanga kitunguu saumu na tangawizi, weka kando.
- Weka mafuta ya maji ya kutosha kwa sufuria kisha kaanga kitunguu hadi kiwe na rangi ya kahawia.
- Ongeza kitunguu saumu na tangawizi kisha koroga hadi viungo vyote vichanganyikane.
- Ongeza nyanya ya mkebe na ukoroge hadi kila kitu kichanganyikane.
- Pika kwa dakika kidogo kisha ongeza nyama iliyochemshwa tayari na ukoroge.
- Ongeza viazi vilivyoshambuliwa tayari na ukoroge hadi viungo vyote vichanganyikane kabisa.
- Pima maji ya mchele kulingana na kiwango cha mchele.
- Maji yakishachemka weka mchele uliooshwa.
- Wacha iive na ikiwa karibu kukauka, funika, punguza moto ili iive pole pole.
- Ikishakauka kabisa, pakua na ule na saladi uipendayo.
Leo nala Pilau basi heheh nimeguzwa na hii recipe
ReplyDeleteEhe niambie, pilau ilikuaje? Ama ilitokea Pilau Njeri...
ReplyDeleteThis I have to try, I hope it will be as good as nyama ya kukaanga.
ReplyDeleteI did it over the weekend ad it was great