Thursday, 12 April 2012

Samaki wa Kukaanga

Viungo:
  1. Samaki au minofu ya samaki
  2. Maji ya limau au ndimu
  3. Chumvi
  4. Kitunguu Saumu
  5. Mafuta ya maji

Kuandaa:
  1. Weka samaki au minofu ya samaki, maji ya limau au ndimu, kitunguu saumu, chumvi kwa bakuli kubwa na uweke kando kwa dakika 20-30.
  2. Weka mafuta ya maji kwa karai kwa moto wa chini.
  3. Toa samaki au minofu ya samaki kwa bakuli ulio na mchanyiko wa maji ya limau au ndimu kisha uweke kwa karai ya mafuta na upike hadi igeuke kuwa rangi ya udhurungi kila upande.
  4. Ikiisha iva epua. 
Pakua na sukuma wiki.

Kuku wa Kupaka

Viungo:
  1. Minofu ya kuku
  2. Vitunguu
  3. Pilipili
  4. Tangawizi mbichi
  5. Mafuta ya maji
  6. Curry Poda
  7. Chumvi
  8. Nyanya
  9. Kitunguu Saumu
  10. Maji ya nazi
Kuandaa
  1. Weka vitunguu, pilipili, tangawizi mbichi na kitunguu saumu kwa kinu na uponde hadi viungo viwe laini.
  2. Ongeza maji. Weka mafuta ya maji kwa sufuria kwa moto wa chini.
  3. Ongeza mchanganyiko wa viuongo ulivyoponda kwa kinu na changanya hadi ziive kwa mda wa dakika 5 hadi 8.
  4. Ongeza nyanya na upike kwa mda wa dakika 3 hadi 4. Kisha ongeza kuku, chumvi, pilipili na maji ya nazi.
  5. Punguza moto na uwache kuku iive kwa mda wa dakika 30.
  6. Ongeza maji.
  7. Ikishaiva epua
Pakua na chapati.


Wednesday, 11 April 2012

Githeri

Viungo:
  1. Mahindi
  2. Maharagwe
  3. Kitunguu
  4. Nyanya
  5. Kitunguu Saumu
  6. Chumvi
  7. Mafuta ya maji
Kuandaa:
  1. Chemsha mahindi na maharagwe pamoja hadi iwe laini.
  2. Kakaanga kitunguu kwa mafuta ya maji kwa sufuria ingine.
  3. Ongeza nyanya na uwache hadi iive, kisha ongeza kitunguu saumu na uwache iive.
  4. Ongeza chumvi na kisha ongeza maharagwe na mahindi uliyochemsha.
  5. Wacha iive kidogo kisha epua kutoka kwa moto.
Pakua na sukuma wiki ikliyokaangwa.

Mukimo

Viungo:
  1. Mahindi changa
  2. Majani ya pumpkin (au kijani mbaazi {green peas})
  3. Viazi
  4. Mafuta ya  maji
  5. Chumvi
Kuandaa:
  1. Chemsha changa hadi iwe laini.
  2. Ongeza viazi vilivyoshambuliwa na majani ya pumpkin lakini usichanganye.
  3. Ongeza chumvi.
  4. Wacha ichemke kwa dakika 30-45 bila kuchanganya.
  5. Ikishaiva, mwaga maji iliyobaki halafu ponda ponda na uhakikishe imepondeka kabisa na imechanganyikana kabisa.
  6. Ongeza mafuta kisha uchanganye.
Pakua na mchuzi wa nyama au kuku.

Pilipili ya Kukaanga

Viungo:
  1. Vitunguu
  2. Nyanya
  3. Kitungu Saumu
  4. Masala
  5. Mafuta ya maji 
  6. Tomato ya mkebe
  7. Maji ya limau
Kuandaa:
  1.  Weka mafuta ya maji kwa kikaangio, kisha ongeza vitunguu wacha iive hadi ikuwe rangi ya udhurungi.
  2. Ongeza nyanya, wacha iive. Kisha ongeza kitunguu saumu na uwache iive.
  3. Ongeza tomato ya mkebe na masala. Punguza moto na uwache iive kwa moto wa chini.
  4. Ongeza maji ya limau, wacha iive kwa moto wa chini.
  5. Epua kutoka kwa moto.
Pakua na chakula chochote.

Wednesday, 19 October 2011

Mchuzi wa Kuku (Kienyeji)

Viungo:
  1. Minofu ya Kuku wa kienyeji
  2. Nyanya mbili kubwa
  3. Kitunguu kimoja kikubwa
  4. Chumvi
  5. Mafuta ya maji
  6. Kitunguu Saumu
  7. Dhania
  8. Pili pili hoho
Kuandaa:
  1. Chemsha kwa mda wa lisaa limoja (Kuku wa kienyeji huwa wagumu na hitaji mda zaidi kufanya walainike).
  2. Ikishalainika na mchuzi umebaki, toa mchuzi na uweke kando.
  3. Kaanga kitunguu kwa mafuta maji hadi kiwe na rangi ya kahawia.
  4. Ongeza kitunguu saumu na chumvi na ukoroge hadi viungo vyote vichanganyikane.
  5. Ongeza nyanya, pili pili hoho na dhania na uongeze kukoroga hadi viungo vyote vichanganyikane.
  6. Ongeza kuku iliyochemshwa na upike kwa dakika kumi hivi.
  7. Ongeza mchuzi uliyoweka kando na uwache iive kwa dakika tano hivi.
Pakua na wali au ugali.

Friday, 14 October 2011

Pilau

Viungo:
  1. Kitunguu
  2. Kitunguu Saumu
  3. Mchele
  4. Tangawizi mbichi
  5. Nyama
  6. Mafuta ya Maji
  7. Nyanya ya mkebe
  8. Viazi
  9. Iliki
  10. Pilau Masala
  11. Mafuta ya maji
Kuandaa:
  1. Chemsha nyama kisha weka kando.
  2. Twanga kitunguu saumu na tangawizi, weka kando.
  3. Weka mafuta ya maji ya kutosha kwa sufuria kisha kaanga kitunguu hadi kiwe na rangi ya kahawia.
  4. Ongeza kitunguu saumu na tangawizi kisha koroga hadi viungo vyote vichanganyikane.
  5. Ongeza nyanya ya mkebe na ukoroge hadi kila kitu kichanganyikane.
  6. Pika kwa dakika kidogo kisha ongeza nyama iliyochemshwa tayari na ukoroge.
  7. Ongeza viazi vilivyoshambuliwa tayari na ukoroge hadi viungo vyote vichanganyikane kabisa.
  8. Pima maji ya mchele kulingana na kiwango cha mchele.
  9. Maji yakishachemka weka mchele uliooshwa.
  10. Wacha iive na ikiwa karibu kukauka, funika, punguza moto ili iive pole pole.
  11. Ikishakauka kabisa, pakua na ule na saladi uipendayo.